Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

King'ongo mambo mswano, barabara, shule ukarabati waendelea kwa kasi ya 4G

7ca2fa5ecee0b72d33725c909702a055 King'ongo mambo mswano, barabara, shule ukarabati waendelea kwa kasi ya 4G

Wed, 20 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

UKARABATI na ujenzi wa shule ya Msingi King’ongo unaendelea kwa kasi huku pia barabara ya kwenda shuleni hapo ikikarabatiwa.

Mtandao huu umeshuhudia tingatinga likichonga barabara kuelekea shule hiyo ambayo miundo mbinu yake ya barabara ilikuwa imeharibika vibaya.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakari Kunenge amesema ukarabati na ujenzi wa Shule ya Msingi King’ong’o utakamilika kwa wakati na kuwa mafundi wanaendelea kufanya kazi usiku na mchana kukamilisha ujenzi huo.

Kunenge amesema viongozi wa Mkoa wamejipanga kuhakikisha ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao hayo na kwamba ukosefu wa madawati nalo wanalishughulikia.

Shule hiyo yenye wanafunzi 2,505 inapatikana katika Kata ya Saranga Wilaya ya Ubungo mkoani Dar es Salaam inahitaji madarasa 45 ambapo kwa kuanza serikali hiyo ya Mkoa imeanza kwa kujenga madarasa manne kwa pamoja.

.

Chanzo: habarileo.co.tz