Arusha. Bodi ya Nyama Tanzana, imeteketeza nyama ya ng’ombe kilo 400 na kumtoza faini ya Sh milioni moja mfanyabiashara Patrick Akyoo katika soko la Samunge baada ya kukutwa akiuza nyama iliyooza.
Akizungumza mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika soko la Samunge, Kaimu Msajili wa bodi hiyo , Imani Sichalwe amesema nyama iliyokuwa inauzwa na mfanyabiashara huyo haikidhi viwango na sheria.
“Ili nyama iuzwe lazima ipigwe muhuri ambao unathibitisha kuwa nyama hiyo imepimwa na daktari na ni sawa kwa mtumiaji na haitaleta madhara kwa jamii, ”amesema
Sichwale amesema mfanyabiashara huyo amevunja sheria za kuuza nyama ikiwamo kufanya biashara hiyo kwenye maeneo machafu, ikiwa siyo mara ya kwanza kwa sababu aliwahi kupewa onyo Mei 19, 2019 lakini amekaidi na kuendelea.
“Tulipita mara ya kwanza tukatoa onyo kwenye bucha zote sokoni hapa ambazo hazijakidhi vigezo ikiwemo hii wenzake walitii kasoro yeye hakutekeleza agizo letu akaendelea kuuza , iwapo atafungua tena tutaifungia leseni yake moja kwa moja,” amesema.
Pia Soma
- Wanaume wakware wapewa dawa ya kutowatamani wanafunzi wa kike
- Uhaba wa walimu kukwamisha ndoto ya Handeni kuwa kinara kwenye elimu
- TPDC yaomba kupunguziwa mzigo wa Deni la Serikali
Amesema jambo lingine ni kuwa na mashine za kukatia nyama na si magogo na nguo za muuzaji ziwe nyeupe na eploni yake iwe ya karatasi inayoweza kufutika na si kitambaa ,kofia na viatu vigumu maarufu kama gambuti.
Amesema mkoa wa Arusha wamekagua bucha zipatao 235 ikiwa zilizofungiwa ni 16 ambapo Samunge 11,Usariver moja kwa Aloyce mbili na Mto wa Mbu mbili kuanzia Mei 11, 2019.
Hata hivyo Afisa mfawidhi kituo cha uchunguzi wa magonjwa ya mifugo kanda ya kaskazini Dk Obedi Nyasebwa amesema nyama hiyo haikuchunjwa ni mzoga, kwani hata rangi ilikuwa tofauti na nyama nyingine.