Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kilio cha mwanamke chamgusa JPM Bahi

076b3fbe8baf7e7e72b9a35be0fdd63e Kilio cha mwanamke chamgusa JPM Bahi

Wed, 3 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

RAIS John Magufuli ameiagiza Halmashauri ya wilaya ya Bahi, mkoani Dodoma kumpa mwanamke, 59, shamba lenye ukubwa wa ekari tano ili apande mikorosho na mazao mengine.

Mwanamke huyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana alimlalamikia Rais Magufuli kwa kuwa alinyang’anywa shamba lao la kikundi ambacho kilikuwa na wanachama 72 bila fidia yoyote licha ya kuwasilisha kilio chao kwa Waziri mwenye dhamana ya ardhi.

Baada ya kumsikiliza, Rais Magufuli aliamuru Halmashauri ya Bahi kumpatia bure shamba la heka tatu mama huyo.

“Sheria ya Ardhi Namba 5....hata kama una plot (eneo) lako la makazi na hujaendeleza unanyang’anywa, ila kwa heshima yako mama, naagiza DC na Mkurugenzi wa Halmashauri hii ya Bahi kumpa shamba ekari tatu mama huyu,” alisema Rais.

Baada ya agizo hilo, Mkuu huyo wa nchi alimwambia mwanamke hiyo: “Mama nakupa heka tatu mlime mazao mengine na mpande mikorosho, nitakuja kuangalia kama mmetekeleza.”

Chanzo: habarileo.co.tz