Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kilimanjaro wapokea Sh15.8 bilioni za maji mwaka mmoja

Maji Huduma Vijijiiiiiiii Kilimanjaro wapokea Sh15.8 bilioni za maji mwaka mmoja

Mon, 21 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (Ruwasa) mkoa wa Kilimanjaro katika mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan madarakani, wamepokea zaidi ya Sh15.8 bilioni kwa ajili ya kutekeleza miradi 37 ya maji katika maeneo ya vijijini.

Miradi hiyo imelenga kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi katika maeneo mbalimbali mkoani hapa ambapo itawezesha upatikanaji wa maji katika maeneo ya vijiji kwa Mkoa huo kufikia asilimia 87.

Hayo yamebainishwa na Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Kilimanjaro, Weransari Munisi wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa maji Kisiwani wilayani Same, ambao umetekelezwa kwa gharama ya zaidi ya Sh500 milioni na unatarajiwa kunufaisha zaidi ya wananchi 10,000 wa eneo hilo.

"Ruwasa Kilimanjaro kwa mwaka mmoja wa Rais Samia tumepata mafanikio makubwa sana Maana kwa mwaka 2021/2022 tumekuwa na bajeti ya zaidi ya Sh15.8 bilioni, hii ni kubwa kuliko miaka mingine yote ambapo tunatekeleza miradi zaidi ya 37".

"Kwa sasa upatikanaji wa maji Kilimanjaro ni asilimia 83 kwa vijijini na tukikamikisha miradi hii tutafika upatikanaji wa maji asilimia 87 kwa maeneo ya vijijini hivyo mwaka huu wa fedha tunavuka lengo la serikali la kufikia asilimia 85 kwa mwaka 2025"

Amesema "Kukamilika kwa miradi hiyo kutanufaisha zaidi ya wananchi 324,797 ambao walikuwa hawana huduma ya maji kabisa na wengine walikuwa wanayo miundombinu lakini ilikuwa imechakaa hivyo tunaboresha iliyochakaa na kuweka miundombinu mipya kwa maeneo ambayo yalikuwa hayana huduma kabisa"

Akizindua mradi wa maji Kisiwani, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Stephen Kagaigai amewaonya wananchi kuacha kuharibu miundombinu ya maji na kuwataka viongozi wa ulinzi kuwakamata wote watakaobainika kuharibu miundombinu na kuwafikisha mahakamani.

"Nimepewa taarifa kuna watu wanakata mabomba, hilo ni kosa na wanaoharibu miundombinu ya maji huo ni uhujumu uchumi wakikamatwa wapelekwe mahakamani, na wananchi wote tushirikiane kuhakikisha miundombinu ya maji inalindwa"amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Same, Edward Mpogolo amesema kwa Wilaya hiyo kwa mwaka mmoja, wamepokea zaidi ya Sh3.8 bilioni kwa ajili ya utekekezaji wa miradi mbalimbali katika Wilaya hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live