Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Kila mtu awe mlinzi vyanzo vya maji’

D751f281067d9472d6eb1fde46d5a2f3.jpeg ‘Kila mtu awe mlinzi vyanzo vya maji’

Sun, 26 Dec 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima amewataka wananchi kulinda na kuvitunza vyanzo vya maji ili viweze kuwa endelevu badala ya jukumu hilo kuliacha kwa serikali na taasisi zinazohusika na usimamizi wa mazingira.

Rai hiyo aliitoa juzi wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maji inayotekelezwa na Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) katika Wilaya ya Korogwe.

Alisema kuwa sio jukumu la serikali pekee kulinda vyanzo vya maji bali ni jukumu la watu wote wanaonufaika na huduma hiyo kwa kuwa waangalifu katika kuvitunza na kuvilinda vyanzo hivyo.

“Tuwe waangalifu katika matumizi ya maji ili yaweze kuwa endelevu kwani Mradi huu wa Rwengera darajani utakapokamilika utaweza kuhudumia watu wengi lakini ni lazima tujenge utamaduni wa kuacha uchafuzi wa vyanzo vya maji ili huduma iwe ni ya kudumu,” alisema.

Naye Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga, Upendo Lu-

gongo alisema kuwa mradi huo wa Rwengera darajani umetengewa fedha kiasi cha Sh mil 660 na unatarajiwa kukamilika ndani ya siku 60 kutoka sasa na wananchi wataweza kupata huduma ya maji safi na salama.

Alisema kuwa mradi huo ni sehemu ya miradi ambayo inatekelezwa katika bajeti ya mwaka 2021/22 ambapo mkoa huo umeweza kutengewa bajeti ya takribani Sh bil 21 kwa ajili ya kutekeleza miradi kwenye wilaya zote za mkoa huo.

“Katika fedha za Covid-19 mkoa umepata Sh bil 6.7 ambazo zitatumika katika

utekelezaji wa miradi ya maji 11 katika wilaya zote za mkoa huu na hivyo kusaidia kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji hususani maeneo ya vijijini,” alisema Lugongo.

Aidha, alisema katika kusogeza huduma ya maji kwa wananchi, Wakala huo umejipanga kuweka huduma ya maji katika maeneo yote ya shule mkoani hapa, hatua itakayosaidia jamii zinazoishi karibu na shule hizo kunufaika na huduma hiyo pia.

“Tunakwenda kuzipatia huduma ya maji ya uhakika shule zote mkoani hapa

ikiwemo kuchimba visima au kusambaza maji ili wanafunzi na walimu waweze kupata huduma hiyo na kuondokana na changamoto za kiafya kutokana na ukosefu wa maji,” alibainisha Meneja huyo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz