Kila baada ya dakika nane, mwanamke mmoja hufariki dunia kutokana na utoaji mimba.
Hii ni licha ya viwango vya vifo vinavyosababishwa na matatizo ya uzazi kupungua kwa theluthi moja katika miaka 20 iliyopita.
Akizungumza katika Kongamano la wadau wa masuala ya Afya ya Uzazi lililoandaliwa na Chama cha Wanasheria Wanawake Tawla, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili(MUHAS), na bingwa wa magonjwa ya wanawake, Profesa Andrea Pembe amesema wanawake katika bara la Afrika ndio wanaongoza kufariki kwa kutoaji mimba usio salama.
Amesema, katika kila dakika moja kuna wamama wanne wanatoa mimba kwa njia ambazo sio salama.
“Na katika kila dakika 8 basi kuna mama ambaye anafariki kutokana na utoaji mimba. Wengine wanashindwa kupata ujauzito kwa sababu ya matatizo ambayo yametokana na utoaji mimba.”Anasema
Anasema wanawake milioni 56 utoa mimba duniani. Watatu kati ya wanne wapo bara la Afrika ambapo wanawake hao wapo hatarini zaidi kupoteza maisha ukilinganisha na mabara mengine.
“Lakini si suala la kufa peke yake katika kila mama mmoja anakufa wengine upata matatizo ya muda mrefu kama ugumba.