Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kikongwe aliyesotea ardhi miaka 42 kutembelewa na Lukuvi leo

65957 Pic+lukuvi

Mon, 8 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini Tanzania, William Lukuvi leo Jumatatu Julai 8, 2019 atamtembelea, Nasi Muruo (98) anayedai ardhi kwa miaka 42.

Akizungumza na Mwananchi leo, Muruo amesema amepata taarifa kuwa Lukuvi atakwenda kumuona, kueleza jinsi anavyomsubiri kwa hamu.

"Mimi ninachotaka ni haki yangu nashukuru sana gazeti la mwananchi na mawakili wangu kunisaidia leo Waziri anakuja," amesema.

Mjane huyo amekuwa akidai kunyang’anywa eneo lake la Sinoni jijini Arusha alilokabidhiwa  na baba yake, Muruo Melusori Februari 5, 1976.

Mwaka 1979 baada ya kunyang'anywa eneo hilo na Edward Lenjashi alikwenda  mahakamani na kushinda kesi lakini tangu mwaka 1979 hajakabidhiwa eneo lake.

Chanzo: mwananchi.co.tz