Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kikongwe aliyepigania ardhi yake kwa miaka 42 kulipwa milioni 500

73327 Mjanepic

Wed, 28 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Hatimaye kaya 109 zimetakiwa kumlipa fidia jumla ya Sh519.3 milioni  kikongwe Nasi Muruo(98) mkazi wa eneo la Sinoni, katika jiji la Arusha, baada ya kurejeshwa ardhi yake aliyokuwa anaidai kwa  miaka 42 .

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo  ya Makazi, William Lukuvi ametangaza leo Jumatano Agosti 28,2019 uamuzi huo wakati akizungumza na kaya hizo na bibi Muruo katika viwanja vya shule ya msingi Sinoni.

Lukuvi alikuwa ameandamana na mkuu wa wilaya Arusha, Gabriel Daqaro na maofisa ardhi katika kutatua mgogoro huo.

Amesema kila kaya italipa kiasi cha Sh20,000 kwa mita moja ya mraba katika eneo la bibi huyo, lakini italipia pia  fedha za kupimwa ardhi ili kupewa hati ndani ya miezi mitatu

Kikongwe huyu alirejeshewa ardhi yake, Julai 8, 2019 na Waziri Lukuvi, kutokana na maelekezo ya Rais John Magufuli wa Tanzania, alipomtaka kushughulikia mgogoro huo, hasa baada ya kuripotiwa malalamiko ya Kikongwe huyo, kunayanyang’anywa ardhi yake tangu mwaka 1977 na ndugu wa ukoo wao, Edward Lenjeshi 

Akizungumza na Mwananchi, Nasi Muruo ameshukuru Rais Magufuli na Lukuvi kwa uamuzi huo ambao umeugwa mkono na pande zote.

Habari zinazohusiana na hii

Wakizungumza katika uwanja wa Sokoni, baadhi ya wamiliki wa viwanja ambao watatakiwa kulipa fidia walisema wamekubali na hawawezi kupingana na serikali.

"Hatupingani na serikali na tunaamini tutapata na kulipa kidogokidogo "alisema Omar Mgaza

Wakili  Hamis Mkindi wa kituo cha sheria na haki za binaadamu(LHRC)  ambao wamekuwa wakimtetea bibi huyo, amesema wanaridhishwa na hatua ambazo zinaendelea kuhakikisha bibi Muruo anapata haki.

Waziri Lukuvi Agosti 8,2019  akizungumza na pande zote katika mgogoro huo, alisema baada ya kazi ya upimaji viwanja katika kaya109  kukamilika, itafanyika tathimini ya kila kaya kumlipa kiasi gani bibi huyo na ambao watashindwa kwa muda utakaowekwa makazi yao yataondolewa na eneo hilo kukabidhiwa bibi huyo.

Hata hivyo, Waziri Lukuvi aliagiza eneo la wazi katika ekari hizo nane, akabidhiwe bibi huyo baada ya kulipima.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz