Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kikongwe aliyechimba madini kwa miaka 42 aiangukia Serikali

Kikongwe Pc Data Kikongwe aliyechimba madini kwa miaka 42 aiangukia Serikali

Tue, 19 Oct 2021 Chanzo: mwananchidigital

Mzee Magembe Mayunga (92) ambaye ni mkazi wa mtaa wa Mchinjioni Manispaa ya Mpanda ameiomba Serikali na wasamaria wema kumsaidia kupata matibabu na mahitaji ya kujikimu.

Mayunga anayeishi na mkewe Selina Nhonoli (62) amesema anasumbuka na maradhi mbalimbali kwa muda mrefu sasa ambapo miguu imevimba na hawezi kutembea wala kula chakula isipokuwa kunywa uji pekee.

Akitoa historia yake kwa Mwananchi Oktoba 16, 2021 nyumbani kwake amesema alikuja Mpanda 1979 akiwa na umri wa miaka 49 kwa ajili ya kufanya shughuli za uchimbaji madini lakini hadi sasa hajawahi kupata dhahabu.

“Nimechimba dhahabu Ibindi na maeneo mengine lakini sijawahi kuipata, niliogopa kurudi nyumbani kwasababu sina hela nilitelekeza familia yangu ya watoto wawili na mke wangu huko Mwagala Simiyu,” amesema.

Mzee huyo anasema tangu ameoanana na mkewe hawajawahi kubahatika kupata mtoto.

“Nilipelekwa hospitali ya Wasabato, nikapimwa na kukutwa na ugonjwa wa kifua kikuu na minyoo. Nilipewa dawa lakini bado naumwa,” anasema.

Kutokana na hali hiyo Mzee Mayunga anawatafuta ndugu zake akiwataja kwa majina ya Kashinje Masaga wa Isaka Kahama na Cheyo Mayunga wa Ng’wandu Meatu waje wamchukue.

Mbali na hilo ameomba watakaoguswa wampatie msaada wa mahitaji na wamsaidie kuwapata ndugu zake kwa kuwa hadi sasa hafahamu familia yake ya watoto wawili na mke wake aliyoiacha Mwagala endapo ipo salama kutokana na muda mrefu kupita.

Akizungumzia hali hiyo, mkewe Selina Nhonoli amesema walioana mwaka 1988 wakiwa eneo la Mpimbwe halmashauri ya Mlele na katika harakati za utafutaji walinunua mashamba na kiwanja kisha kujenga makazi Mpanda Hoteli.

“Kabla ya kuugua nilikuwa namwambia twende nyumbani kwenu anakataa hii ni mara ya pili kuugua ya kwanza nilihangaika naye akapona awamu hii hali ni tofauti amezidiwa.

“Anaomba ndugu zake waje mie siwafahamu sielewi nitawapataje, majirani hawatusaidii chochote isipokuwa mmoja tu, nilitoa taarifa kwa mjumbe ili nipatemsaada,” anasema akiwashukuru Wasabato waliowaletea unga wa uji.

Kwaupande wake Mjumbe wa Serikali ya mtaa huo, Onesmo Bugota amekiri kupokea taarifa za ugonjwa wa mzee Magembe na alifika na kushuhudia hali hali ilivyo.

“Nilimuuliza mke wake ndugu zake wako wapi akadai hawafahamu, lakini hawa wazee wana hali ngumu ya kimaisha naomba Serikali itoe msaada na wanadungu popote walipo wajitokeze,” amesema Bugota.

Mmoja wa majirani wa familia hiyo Elizabeth Ngasa amesema amekuwa akitoa msaada kwa mgonjwa huku akiiomba serikali na wasamaria wema wakiwamo majirani watoe msaada wowote.

Chanzo: mwananchidigital