Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kijiji chaamua: Usipomsindikiza mke kliniki faini Sh50,000/-

MIMBA W Kijiji chaamua: Usipomsindikiza mke kliniki faini Sh50,000/-

Thu, 5 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KIJIJI cha Neruma wilayani Bunda mkoani Mara kimepitisha sheria ndogo inayowalazimisha wanaume kuwasindikiza kliniki wenza wao kipindi cha ujauzito.

Akizungumza katika mahojiano maalum na HabariLeo, Mtendaji wa Kijiji cha Neruma, Mwalimu Kapei Laizer Lazaro amesema katika kikao cha wananchi kilichofanyika katika Kijiji hicho kimepitisha faini ya Sh 50,000 kwa mwanaume kutompeleka kliniki mwenza wake.

Pia, mwanamke akijifungulia njiani faini ni Sh 50,000 na akijifungulia kwa mkunga wa jadi faini ni Sh 200,000.

Amesema wameweka faini hizo ili kupunguza vifo vya wajawazito na Watoto ambavyo vimekuwa vikikithiri katika Kijiji hicho kutokana na changamoto mbali mbali ikiwemo uchelewaji wa kuwahi kufika kituo cha afya, na kutohudhuria kliniki kipindi cha ujauzito.

“Hapa tuna kituo kikubwa cha afya cha Kasaunga ambacho kinahudumia vijiji vitano, kwa pamaja tumejiwekea sheria hii ili kuwahimiza wanaume kushiriki katika malezi ya Watoto kuanzia tumboni, kama mama anasahau kunywa dawa za kuongeza damu basi baba atamkumbusha, watapata pamoja elimu ya uzazi wa mpango na elimu ya lishe, hii inawasaidia katika ukuaji wa mtoto.”Amesema Laizer

Aidha, amesema wamekuwa wakitoa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana ili kuwasaidia mabinti kuepuka mimba za utotoni na wale ambao tayari wamebeba mimba zisizotarajiwa wanapewa elimu ya uzazi wa mpango ili wasirudie makosa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live