Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kijana usipolima korosho utakamatwa

KOROSHOO Kijana usipolima korosho utakamatwa

Tue, 24 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Halmashauri ya Wilaya ya Momba imetoa onyo na tahadhari kwa Vijana ambao watashindwa kulima kilimo cha korosho na ufuta kwamba watakamatwa na Serikali za Vijiji vyao na watapewa adhabu ya kwenda kulima kwenye mashamba ya wenzao waliolima ufuta na korosho, bila kulipwa chochote.

Hatua hii inatokana na Serikali ya Halmashauri ya hiyo kuja na mkakati wa kutoa elimu na kuhimiz kila Mwananachi mwenye umri kuanzia miaka 18 kuchangamkia fursa ya kilimo cha ufuta na korosho ambacho kimeonekana kufanya vizuri na kwa tija kwa Wakulima wa Momba.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Momba, Methew Chikoti amesema hayo wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi na kusikiliza kero za Wananchi akiambatana na Madiwani wa Kamati ya Fedha, Mipango na Uongozi.

Chikoti amesema Halmashauri imejipanga na imeishaandaa mbegu bora za ufuta na korosho kwa ajili ya kuwagawia Wananchi kwa utaratibu mzuri ambao umepangwa na Wataalamu.

"Tunataka kuona kila kaya ndani ya Momba inalima ekari moja ya ufuta au zaidi na kwa zao la korosho lengo letu ni kuona kila kaya inaandaa na kulima nusu eka ya korosho ili Wakulima wetu wapate fedha kupitia mazao aya na kuondokana kutegemea kilimo cha mpunga na mahindi, lengo letu ni kuona kila mmoja analima na kupata fedha kwa ajili ya kukuza uchumi wa Familia yake pamoja na wa Halmashauri ya Mombaā€¯.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live