Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kijana mwingine akutwa amejinyonga Iringa

Maiti Mauaji Kifo 58 Instagram Kijana mwingine akutwa amejinyonga Iringa

Wed, 6 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwili wa mwanaume ambaye jina lake bado halijatambulika amekutwa amejinyonga karibu na Shule ya Sekondari ya Bethel iliyopo katika Mji wa Mafinga usiku wa kuamkia machi 4, 2024.

Akitolea ufafanuzi wa tukio hilo Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mufindi, Antony Gwandu amesema alipata taarifa hizo wakati akielekea kazini na baada ya kufika katika eneo la tukio alikuta mtu huyo amejinyonga na kueleza kuwa uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na baada ya kukamilika taarifa rasmi itatolewa na msemaji wa polisi Mkoa wa Iringa.

Hata hivyo mwili huo umebebwa na polisi kwa ajili ya taratibu za kiuchunguzi huku upelelezi wa tukio hilo ukiwa bado unaendelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live