Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kijana aporwa na kuuawa Dar

Kamanda Muliro Panyaz.jpeg Kijana aporwa na kuuawa Dar

Thu, 6 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkazi wa Mwananyamala, Manjunju mkoani Dar es Salaam, Billal Hoza (21), amefariki dunia baada ya kuvamiwa na kundi la vijana waliomchoma kisu sehemu mbalimbali za mwilini na kumpora simu.

Vijana hao wapatao watano walimvamia kijana huyo aliyekuwa amekaa nje ya nyumba yao na kumchoma kisu mgongoni, upande wa moyo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea juzi saa 3:30 usiku, wakati Hiza na rafiki yake wakiwa wamekaa barazani nyumbani kwao, wakichezea simu.

“Wakati wanachezea simu walipita vijana kama wanne, kati yao mmoja akamfuata huyu kijana (Hoza) akampokonya simu, akaendelea kutembea na wenzake, ndipo Hoza akamfuata, akambana na kumtupa chini na mmoja wao akatoa kisu na kumchoma mgongoni, wakaendelea kutembea,” Kamanda Muliro.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live