Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kijana aliyepanda kwenye nguzo za umeme mkubwa azua taharuki

NGUZO UMEMEEE Kijana aliyepanda kwenye nguzo za umeme mkubwa azua taharuki

Fri, 20 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mhandisi wa usafirishaji umeme mkoa wa Mwanza na Mara Shakiru Abdallah, amesema kwamba kijana aliyekuwa amepanda juu ya nguzo ya umeme wa msongo wa kilovoti 132 namba 500 kwenye njia ya Mwanza- Musoma iliyopo Mwibagi Wilaya ya Bunda Mkoa wa Mara, anakabiliwa na changamoto za matatizo ya afya ya akili.

Kijana huyo Nzungu Ndaki anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 hadi 30, alifanya tukio hilo jana Januari 19, 2023, na kwamba kwa mujibu wa shemeji yake kijana huyo alikuwa akipatiwa matibabu ya kienyeji.

Aidha, Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kiabakari wilayani Musoma alifanikiwa kufika eneo la tukio mapema na kuamuru kufanyika kwa maamuzi magumu ili kumuokoa kijana huyo.

"Timu yetu imefika na kumshawishi mhusika kushuka bila mafanikio. Jitihada za kumshusha bila kudhurika zinaendelea, na tunaweza kulazimika kuzima laini hiyo ambayo itapelekea Mkoa wote wa Mara kukosa umemeā€¦"

Akizungumzia tukio hilo, Mhandisi Shakiru, amesema kuwa hata hivyo zoezi la kumshusha lilifanikiwa baada ya kupata kibali cha kuzima umeme kwa muda, na kwamba alikabidhiwa kwa mamlaka za Jeshi la Polisi mkoani Mara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live