Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kijana aliyeokoa abiria wa ndege alivyoondoka kupelekwa jeshini

WhatsApp Image 2022 11 08 At 12.jpeg Kijana aliyeokoa abiria wa ndege alivyoondoka kupelekwa jeshini

Tue, 8 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kijana Majaliwa aliondoka katika Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba baada ya kumalizika kwa zoezi la kuaga miili ya watu 19 waliopoteza maisha katika ajali ya ndege ya Precision Air iliyoanguka Ziwa Victoria baada ya kushindwa kutua juzi Asubuhi.

Majaliwa ambaye ni mvuvi ameondoka akiongozwa na Kamanda wa Mkoa wa Kizimamoto Mwanza.

Ikumbukwe Baada ya Ushujaa Aliouonyesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameagiza kijana huyo akabidhiwe kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ili atafutiwe nafasi kwenye Jeshi la Uokozi.

Majaliwa alisaidia kufungua mlango wa ndege ya Precision Air iliyozama ziwa Victoria kwa ajili ya kuokoa abiria waliokuwa ndani yake ambapo walifanikiwa kuokoa watu 24, huku watu 19 wakipoteza maisha.

Awali Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa alimkabidhi kijana huyo shilingi milioni moja kama zawadi kutokana na Ujasiri wake katika tukio hilo.

"Ndege ile ilikuwa na abiria 43, katika hao 39 ni wasafiri, wawili ni wahudumu na wawili mmoja ni rubani na mmoja ni msaidizi wake. Waliofariki ni 19 na waliookolewa katika ajali waliokuwa wasafiri ni 24 na sio 26 kama ambavyo tuliripoti jana (juzi).

"Kijana mmoja aliyejitupa ndani ya maji na ndiye aliyechukua ile kasia na kufungua ule mlango, kwa bahati mbaya na yeye aliumia akazirai na wenzake wakamuokoa na alipofika hospitali walimjumuisha kuwa ni watu waliokuwa ni wasafiri, anaendelea vizuri sasa" alisema.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa gharama za mazishi ya waliofariki yote yatagharamiwa na serikali ya Tanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live