Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kijana ajitokeza kuuza Figo "maisha ni magumu"

Kijana Na Figo Paul Phocus, anayeuza Figo yake

Wed, 15 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Paul Phocus (22) mkazi wa Dar es Salaam amesema kutokana na hali ngumu ya maisha yupo tayari kujitolea Figo yake moja kuiuza ili apate fedha za kujikimu yeye na familia yake.

Paul ambaye amekiri kutokuwa na uelewa zaidi kuhusu utoaji wa Figo, ameeleza kuwa amekuwa akihangaika kutafuta kazi bila kupata hali iliyomsukuma kushawishika kuuza Figo yake.

Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani na Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Daniel Msilanga, ameeleza kuwa kwa utaratibu wa sasa nchini mtu akihitaji Figo, ndugu zake wa damu ndiyo huruhusiwa kumpa Figo.

Wabunge kama Faustine Ndugulile na Mbunge wa Viti Maalum Rose Tweve wameshawahi kunukuliwa wakitaka muswada wa uvunaji wa viungo vya binadamu kama Figo kupelekwa bungeni huku serikali kupitia Wizara ya Afya ikikiri kuwa ipo mbioni kuandaa muswada huo, ili sheria iruhusu uvunaji wa viungo hivyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live