Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kijana adaiwa kuua muombolezaji msibani

Mauaji Abc.jpeg Kijana adaiwa kuua muombolezaji msibani

Fri, 19 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkazi wa kitongoji cha Faru, Mji mdogo wa Himo mkoani Kilimanjaro, Godbless Kawiche (26), anadaiwa kumuua kwa kumkata na kitu chenye ncha kali na kumchoma moto mmoja wa waombolezaji aliyekuwepo kwenye msiba wa kaka yake.

Tukio hilo limetokea leo, Alhamisi Januari 18, 2024 kwenye msiba wa Gift Kawiche aliyefia Mombasa nchini Kenya baada ya kupata ajali ya shoti ya umeme iliyosababisha kuanguka na hatimaye alifariki Jumanne Januari 16, 2024.

Mwili wa Gift Kwiche utawasili kesho nyumbani kwao kwa ajili ya taratibu za maziko ambayo yatafanyika Jumamosi, Januari 20, 2024.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa alipotafutwa kuthibitisha tukio hilo ambapo amesema yupo nje ya mkoa na kuagiza atafutwe Kaimu kamanda wa mkoa huo, Abel Mtagwa ambaye amekiri kuwepo kwa tukio hilo lipo na kwamba atalitolea.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Faru, Erasmus Assey, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, akisema limetokea alfajiri leo, Alhamisi Januari 18, 2024.

Akisimulia jinsi tukio hilo lilivyotokea, Assey, amesema wakati baadhi ya waombolezaji wakiwa wanakesha kwenye msiba huo, kuliibuka sintofahamu baada ya mdogo wa marehemu, Godbless Kawiche kuanza kuwafukuza waombolezaji.

Amesema, wakati anaendelea na vurugu hizo, palitokea mzee mmoja mwenye umri kati ya miaka 70-75 jamii ya Kimaasai aliyekuwepo msibani hapo ambaye alipatwa na usingizi, ambapo kijana huyo alimtaka kwenda kupumzika chumbani kwake.

“Vurugu zilikuwa zinaendelea, huku waombolezaji waliokuwepo msibani hapo pamoja na wazazi wake wakikimbia kwenda kuomba hifadhi jirani,” amesema.

Amesema waombolezaji walijaribu kumzuia kijana huyo huku wakimsihi aombe radhi kwa waombolezaji aliowaletea vurugu.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa kijana huyo alirejea kufanya vurugu, akianza kuwafukuza tena waombolezaji na ndipo baba yake alikwenda Polisi kuomba msaada na huko alipewa RB na askari waliofika kumdhibiti kijana huyo na kumfunga pingu.

"Wakati wanasema waangalie ni kitu gani ameharibu, wakakutana na sehemu kuna dimbwi la damu, wakauliza ni nini kimetokea?

“Kuangalia huku na kule kukawa kuna mahali kulikuwa kumewashwa moto wakakuta mwili wa mtu umechomwa moto,” amesema.   Mwenyekiti huyo, amesema aliyeuawa ni yule mzee aliyeambiwa akapumzike na kijana aliyekuwa akifanya vurugu na inaonekana aliburuzwa umbali wa mita 10 baada ya kuchomwa moto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live