Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kigugumizi Sh600 milioni zilizojenga shule Longido

Pesa Fedhaddd Kigugumizi Sh600 milioni zilizojenga shule Longido

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Madini Dk Steven Kiruswa, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Longido mkoani Arusha, amekataa kuchangia ujenzi wa shule ya Msingi Mundarara, mpaka apate maelezo ya kina matumzi ya fedha Sh mil 600 zilizotumwa na Serikali katika ujenzi wa shule hiyo.

Kiruswa amesema hayo baada ya kutembelea shule hiyo na kujionea ujenzi wa madarasa nane, ofisi ya utawala,vyumba vitatu vya maabara na vyoo havijamaliziwa na nyumba ya mwalimu mkuu haijajengwa, milango hakuna na sakafu haijamaliziwa na tayari zimetumika zaidi ya shilingi milioni 576.

Amesema ameambiwa fedha zilizobaki katika akaunti ni shilingi milioni 8 tu na bado shule haijakamilika kabisa.

Amesema katika kata zingine jimboni Longido, fedha za serikali zilizopelekwa katika katika Kata nyingine jimboni humo zimetumika vizuri na shule zimekamilika.

Naibu Waziri amesem kutokana na hali hiyo hawezi kuchangia chochote, hadi ufanyike ukaguzi maalumu wa matumizi ya fedha zote zilizotumika na apate majibu, kwani Kamati ya Ujenzi wa shule hiyo haikushirikishwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live