Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kigoma yatamba Umitashumta

647b7c4307566bbccd5b2b3816104b86.jpeg Kigoma yatamba Umitashumta

Mon, 14 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MIKOA ya Manyara na Kigoma imetamba katika mashindano ya Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi Tanzania (Umitashumta) yanayoendelea mkoani Mtwara kwa kuongoza katika mchezo wa kurusha tufe.

Kwa mujibu wa Msemaji Mkuu wa mashindano hayo, John Mapepele, mkoa wa Manyara unongoza katika mchezo huo kwa upande wa wasichana, huku mkoa wa Kigoma ukiongoza kwa upande wa wavulana.

Kwa upande wa wasichana, mshindi wa kwanza ni Rebecca Muhakla kutoka Manyara aliyerusha tufe umbali wa mita7 na sentimeta 90, huku mshindi wa pili akiwa Mariam Festi kutoka mkoani Pwani aliyetupa tufe umbali wa mita 7 na sentimeta 60.

Mapepele aliliambia HabariLEO kuwa, Mwanaidi Yassin kutoka mkoani Singida alikuwa mshindi wa tatu kwa kutupa tufe umbali wa mita 7 na sentimeta 46.

Mapepele ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, aliwataja washindi wa mchezo huo kwa upande wa wavulana kuwa ni Emmanuel Michael kutoka mkoani Kigoma aliyerusha tufe umbali wa mita 10, akifuatiwa na Fadhili Mwampote kutoka Mbeya aliyefikisha mita 9 na sentimeta 99.

Mshindi wa tatu kwa mujibu wa Mapepele ni Abbasi Muhidin kutoka mkoani Pwani aliyerusha tufe hadi umbali wa mita 9 na sentimeta 88.

Chanzo: www.habarileo.co.tz