Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kigoma yafikia asilimia 90 chanjo ya Uviko-19

MBEYA CHANJO Kigoma yafikia asilimia 90 chanjo ya Uviko-19

Thu, 21 Oct 2021 Chanzo: ippmedia.com

MKOA wa Kigoma umefikia asilimia 90.7 ya uchanjaji wa chanjo ya UVIKO-19 kwa chanjo ya J &J zilizo pokelewa mapema mwezi Agosti mwaka huu.

Akielezea kuhusu mwenendo wa utoaji chanjo hiyo kaimu mratibu wa chanjo Mkoa wa Kigoma, Henry Kisinda amesema walipokea dozi 37,000 na hadi kufikia takwimu za jana watu 33,569 wamechanjwa.

Ameeleza tangu kuanza kwa utoaji chanjo Agosti 03 hadi Septemba 23 mwaka huu ni watu 3,028 tu ndio walikuwa wamechanjwa sawa na asilimia 8.2 ya dozi walizo pokea, lakini kuanza kwa klinik tembezi  mwishoni mwa mwezi Septemba kumewezesha watu 30,541 kuchanjwa sawa na ongezeko la asilimia 82.5 .

Ameeleza hatua hiyo ina ashiria wananchi wanaikubali chanjo hiyo na wako tayari kuchanjwa ila hawakuwa na elimu pamoja na wengine kukwamishwa na umbali wa kufuata huduma hiyo.

"Watu wako tayari kuchanjwa,sema kama mtu haumwi ni ngumu kwenda kwenye kituo cha kutolea huduma" amesema Kisinda.

Awali mwazo wa zoezi hilo serikali ya mkoa ilikuwa na vituo 24 sawa na mgawanyo wa vituo vitatu kila halmashauri na baadae kuongezwa hadi kufikia 254.

Pia takribani wahudumu wa afya ngazi ya jamii 920 walipewa mafunzo ya chanjo ya UVIKO 19  na wanaendelea na uhamasishaji katika jamii zao.

Chanzo: ippmedia.com