Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kigoma: Asilimia 40 ya waliopimwa wana tatizo la moyo

MOYO Darrrr Kigoma: Asilimia 40 ya waliopimwa wana tatizo la moyo

Fri, 19 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu 11,200 wamefanyiwa vipimo vya magonjwa ya moyo nchini, ambapo asilimia 40 kati yao wamegunduliwa kuwa na tatizo la magonjwa hayo hivyo kuanzishiwa utaratibu wa matibabu.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dk Eva Mganda, amesema hayo wakati wa kliniki ya siku tatu ya upimaji wa awali ya magonjwa ya moyo kwa wananchi wa Mkoa Kigoma inayofanyika Hospitali ya Mkoa Kigoma Maweni.

Amesema katika upimaji huo uliofanyika asilimia 12 ya watu hao waligunduliwa kuwa na changamoto kubwa ya magonjwa ya moyo, hivyo kuhitaji huduma za dharura za matibabu hivyo kufanyiwa taratibu za kupata huduma zaidi za kibingwa na kwamba changamoto kubwa ipo kwa watu kuchelewa kuanza upimaji na hivyo kuhitaji rufaa ya dharura kwa ajili ya kupata matibabu ya kibingwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live