Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kigamboni watakiwa kujitolea kuboresha miundombinu

28230 Pic+kigamboni TanzaniaWeb

Thu, 22 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakazi wa Kigamboni wametakiwa kujitolea kushirikiana na Serikali katika kuboresha miundombinu ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza wakati wa mvua.

Kauli hiyo imetolewa leo Novemba 21 na mkuu wa wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri wakati wa ziara ya kukagua maeneo yanayoathirika wakati wa mvua.

Amesema kwa kuwa mipango ya manispaa hiyo ni ya muda mrefu kuelekea kipindi cha mvua za vuli na masika wananchi wanatakiwa kujitolea ili kuepukana na maafa.

"Tunajua kuna mipango ya muda mrefu ili kuboresha manispaa yetu tukiwa tunasubiri michoro hiyo tujitolee kushirikiana na Serikali ili tuweze kuondokana na changamoto hiyo," amesema Msafiri.

Amesema hawezi kuwa anatoa pole kwa waathirika wakati wananchi wanaweza kujitolea kushirikiana na Serikali kunusuru maafa yasitokee.

"Wako wananchi wenye uwezo wa kujitolea nguvu kazi, kwa kushirikiana na ofisi yangu tutahakikisha safari hii hakutokei maafa wakati wa mvua," amesema.

Akielezea chanzo cha mafuriko mkazi wa mtaa wa Kichangachui Sabia Ally amesema chanzo cha mafuriko kwa baadhi ya maeneo ni pamoja watu kuvamia maeneo ya wazi na kujenga juu ya miundombinu.

Amesema baadhi ya maeneo ya wazi wakati wa mvua maji yalikuwa yakitiuama lakini kutokana na ujenzi holela maji yamekuwa yakisambaa kwenye makazi ya watu.

"Kwa kipindi cha nyuma kero ya mafuriko haikuwepo lakini baada ya watu kujenga maeneo ya wazi na kwenye miundombinu kero hii imeongezeka," amesema Sabia.



Chanzo: mwananchi.co.tz