Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kifo cha msomi UDSM chaibua maswali, binti yake asema...

91126 Pic+kifo Kifo cha msomi UDSM chaibua maswali, binti yake asema...

Wed, 8 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kifo cha msomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nchini Tanzania, Profesa Amon Mbelle (66) kimeibua maswali.

Profesa Mbelle aliyekuwa anaishi mtaa wa Nyanza, Kunduchi Mtongani jijini Dar es Salaam, alikutwa amefariki dunia Jumapili ya Januari 5, 2020 saa 4:00 usiku chumbani kwake.

Katika familia hiyo, yenye jengo la ghorofa mbili, alikuwa anaishi peke yake pamoja na walinzi wawili, Ali Selemani na Michael aliyefahamika kwa jina moja.

Msaidizi mwingine ni msichana na kazi, Yasinta aliyekuwa anakuja na kuondoka hapo nyumbani.

Akizungumza nyumbani hapo leo Jumanne Januari 7, 2020 Phillo Mbelle, kaka wa marehemu Profesa Mbelle amesema alikuwa anaishi nao kwa zaidi ya miaka saba tangu alipotengana na mkewe.

Maswali yanayoibuka kuhusu kifo chake yanachagizwa na taarifa zilizosimuliwa na mtoto wake wa kwanza, Josina Mbelle.

>Josina aliyepewa taarifa hizo na mlinzi wake Ali alisema marehemu Profesa Mbelle alirejea nyumbani saa 11:00 jioni na kuelekea kupumzika chumbani kwake.

"Alipoingia ndani hakujua tena kinachoendelea, baada ya muda Ali (mlinzi wake) akaenda kugonga kwa sababu alimpatia maelekezo ya kufanya," alisema Josina.

"Walivyoona kimya baadaye wakatoa taarifa polisi, saa nne usiku hivyo wakavunja mlango na kukuta mwili wake uko chini, akiwa na damu usoni nadhani alidondoka kitandani."

Amesema mwili wa Profesa Mbelle utazikwa kesho Jumatano katika makaburi ya Kondo, hakuwahi kulalamika afya yake kwa siku za karibuni kabla ya mauti.

Pia, alikuwa mtu wa mazoezi kulinda afya yake.

Hata hivyo, kaka yake, Phillo Mbelle amesema kabla ya kurejea nyumbani, alikuwa moja ya sehemu za vinywaji akiwa na rafiki zake, yeye hakunywa pombe siku hiyo licha ya kuwa mtumiaji.

"Yeye hakunywa pombe anavyosema, lakini huwa nakunywa, " amesema.

Haikuwa rahisi kuzungumza na mke wa marehemu lakini Josina amesema familia haioni sababu za kufanya uchunguzi wa kifo chake.

"Familia tunaamini ni kifo cha kawaida tu, tunamwachia Mungu," amesema Josina mtoto wa kwanza kati ya watoto wake watano aliowaacha hai.

Kwa niaba ya familia hiyo, Josina amesema ni majonzi yatabakia kwao kutokana na ukaribu, upole na ucheshi wa marehemu baba yao

Mmoja kati ya wafanyakazi wenzake, kutoka Idara ya rasilimali watu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ramadhani Bomba amesema alimfahamu marehemu tangu mwaka 1983 kabla ya kujiendeleza kielimu.

"Kwa ufupi tumefanya kazi miaka yote hiyo alikuwa ni mcheshi, mtu wa kujali watu sana, alikuwa mshauri wa karibu sana unayetamani kumsikiliza tu," amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz