Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kifo cha mfanyakazi wa ndani Arusha chawaibua watetezi Mwanza

Kifo cha mfanyakazi wa ndani Arusha chawaibua watetezi Mwanza

Fri, 13 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Mashirika na taasisi za utetezi wa haki za binadamu jijini Mwanza nchini Tanzania yameiomba Serikali kuridhia mkataba namba 189 wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) kuhusu kazi za staa kwa wafanyakazi wa nyumbani kuwawekea mazingira bora na salama kazini.

Ombi hilo limetolewa jijini Mwanza leo Ijumaa Machi 13, 2020 na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la WoteSawa linalotetea haki za wafanyakazi wa majumbani, Angela Benedicto alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kifo cha Salome Zacharia (17) kinachodaiwa kutokana na kipigo kutoka kwa mwajiri wake kwa tuhuma ya wizi wa Sh50, 000.

Akizungumza kwa niaba ya mashirika mengine saba, Angela amesema kuridhiwa kwa mkataba huo kutowezesha uwapo wa sheria na kanuni zitakazoweka viwango bora na salama kwa kazi za nyumbani, haki na wajibu ya waajiri na wafanyakazi.

"Tafiti zinaonyesha kuwa wafanyakazi wa nyumbani ni miongoni mwa kundi lisilotambuliwa katika mifumo rasmi ya ajira; hii inasababisha ukatili, unyanyasaji, mateso na kudharaulika licha ya umuhimu na majukumu ya katika familia wanazohudumu,” amesema

Amesema pamoja na vipigo, kada hiyo pia inakabiliwa na tatizo la kutopata ujira stahiki na kwa wakati ambapo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, WoteSawa imepokea na kushughulikia mashauri 660 ya ukatili na unyanyasaji kijinsia dhidi ya wafanyakazi wa ndani katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

“Mashauri mengi yalihusu wafanyakazi wa nyumbani ambao wengi wao wana umri chini ya miaka 18 ni kutolipwa mishahara, kupigwa, kudhalilishwa na unyanyaswaji wa kingono kutoka kwa waajiri, ndugu, jamaa na marafiki wa familia,” amesema

Pia Soma

Advertisement
Mashirika mengine yaliyotoa ombi hilo ni pamoja na Tanzania Domestic Workers Coalition (TDWC), Kiota Women Health and Development Organisation (KIWOHEDE), Mwanza Youth and Children Network (MYCN), Ndenuka Organisation, Haki zetu Organisation, Nuru Organisation, HAWA na Wanawake Live.

Chanzo: mwananchi.co.tz