Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kifo cha dereva wa basi safarini chaibua hofu

99775 Pic+dereva Kifo cha dereva wa basi safarini chaibua hofu

Thu, 26 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza/Shinyanga. Siri ya kifo ajuaye ni Mungu pekee! Hivyo ndivyo kinavyoweza kuelezwa kuhusu tukio la dereva wa kampuni ya mabasi ya Isamilo ya jijini Mwanza, Sebastian Mathias (43) kilichotokea ndani ya basi akiwa safarini kutoka Mbeya kwenda jijini Mwanza.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Deborah Magiligimba alisema kifo cha dereva huyo kilichoibua hofu miongoni mwa wafanyakazi wenzake na abiria kiligundulika alipofikishwa Kituo cha Afya Tinde mkoani Shinyanga.

Akizungumza na Mwananchi kwa simu jana kuhusu kifo hicho, mwenyekiti wa chama cha wamiliki wa mabasi Kanda ya Ziwa, Rogers Malaki alisema taarifa za kifo hicho zimewashtua wadau wa sekta ya usafirishaji kutokana na mazingira yake.

“Kama chama tayari tumepata maelezo kutoka kwa mwajiri kuwa kabla ya kifo chake, dereva huyo hakutoa taarifa yoyote rasmi ya kiofisi kuhusu kuumwa kwake. Kampuni ya Isamilo ina utaratibu wa kutoruhusu mfanyakazi mwenye tatizo la kiafya kusafiri,” alisema Malaki.

Mmoja wa wadau wa sekta ya usafirishaji abiria jijini Mwanza, Masoud Masasi aliiambia Mwananchi kuwa watumishi wengi wa mabasi ya mafasa marefu wanakabiliwa na tatizo la uchovu kutokana na kufanya kazi mfululizo bila kupumzika.

“Baadhi ya madereva na makondakta wanaweza kufanya kazi mfululizo hata miezi mitatu; wanachofanya wakifika mwisho wa safari wanapumzika saa chache,” alisema.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement

Kazini dakika za mwisho

Kamanda Deborah alisema dereva huyo alianza kujisikia vibaya tangu mwanzo wa safari kutokea Mbeya, lakini alijitahidi kuendesha hadi walipofika Singida na kumkabidhi mwenzake na hali yake ilibadilika na kujisikia vibaya zaidi.

“Wakati mwenzake aliyempokea Singida akiendelea kuendesha, Sebastian alijipumzisha lakini hali yake ilibadilika zaidi walipofika Tinde na kupelekwa kituo cha afya kwa matibabu lakini daktari aligundua alishafariki dunia,” alisema.

Alisema kifo cha dereva huyo kiligundulika jana saa 4:00 asubuhi na mwili wake kuhifadhiwa Kituo cha Afya Tinde.

Chanzo: mwananchi.co.tz