Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kicheko fedha miradi ya afya, maji kuongezwa

Kahama Maji Kicheko fedha miradi ya afya, maji kuongezwa

Sun, 27 Aug 2023 Chanzo: eatv

Madiwani wa Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama, Shinyanga wamemwagiza mkuu wa wilaya hiyo Mboni Mhita na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mary Mhoha kufikisha salamu za pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Hii ni kutokana na kuongezeka kwa fedha za kuimarisha sekta ya elimu, afya, barabara, maji na nishati ya umeme vijijini kupitia mradi wa REA katika halmashauri hiyo.

Kauli hiyo imetolewa wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo madiwani, wakuu wa idara na vitengo katika ukumbi wa halmashauri hiyo mwishoni mwa wiki.

Hoja ya pongezi kwa Rais Samia kwa niaba ya madiwani wa halmashauri hiyo, ilitolewa na Diwani wa Kata ya Mwakata, Sixbert Ibrahim ambapo iliungwa mkono na madiwani wote waliohudhuria mafunzo hayo.

Katika mafunzo hayo Mhita alimpongeza mkurugenzi wa halmashauri hiyo Khamis Katimba kwa jitihada na mikakati yake aliyoionesha katika muda mchache tangua aingie kwenye halmashauri hiyo.

“Halmashauri imepata mtu makini sana, tuungane naye kuhakikisha malengo yake mapana yanafikiwa. Kwa muda mchache tumeona mwelekeo wake chanya,” Amesema.

Kwenye mafunzo hayo, Mhita pia alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme kwa kukubali ombi la kutoa wakufunzi wawili kuwezesha mafunzo hayo kwa lengo la kuongeza ufanisi katika kusimamia miradi ya maendeleo.

Chanzo: eatv