Tue, 8 Nov 2022
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Watu saba ambao ni watumishi wa serikali ya wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara Idara ya afya na elimu wamefariki dunia kwa ajali baada ya gari waliyokuwa wamepanda kugongana na gari lingine aina ya Toyota Prado katika eneo la Pori namba moja Kata ya Partimbo wilayani Kiteto mkoani Manyara.
Katika ajali hiyo watu wengine watano wamejeruhiwa na wamehamishwa kwenda hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu zaidi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, RPC George Katabazi amethibitisha kunusurika kwa kichanga katika ajali hiyo.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live