Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kibiki aondolewa uenyekiti halmashauri ya Babati

41661 Kibitipic Kibiki aondolewa uenyekiti halmashauri ya Babati

Thu, 14 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Babati. Baraza la madiwani halmashauri ya mji wa Babati mkoani Manyara limemuondoa kwenye uongozi mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Mohamed Kibiki (Chadema) kwa maelezo ya kushindwa uongozi.

Kibiki ameondolewa baada ya kupigiwa kura kwenye kikao cha baraza hilo leo Jumatano Februari 13, 2019. Kati ya kura 12 zilizopigwa, wajumbe nane walimkataa na wanne walitaka aendelee na uongozi.

Mbunge wa Babati Mjini (Chadema), Pauline Gekul amesema mwenyekiti huyo aliondolewa kwenye nafasi hiyo baada ya kushindwa kuongoza.

Amesema baada ya kubaini tuhuma zake mbalimbali waliamua kumuondoa kwa kupiga kura ya kutokuwa na imani naye.

Amebainisha kuwa si lazima mwenyekiti kukaa katika yake kwa miaka mitano bila kuondolewa kwa maelezo kuwa kanuni zinaruhusu endapo inaonekana amekiuka utendaji wake wa kazi.

Gekul amesema mwenyekiti huyo alishindwa kuisimamia halmashauri hiyo, alifanya mambo kwa maslahi yake binafsi.

Amesema zaidi ya vitabu 60 vya nakala ya mapato ya halmashauri hiyo vimepotea na mkurugenzi huyo akiagizwa afuatilie, amekuwa akiwatetea wahusika.

Akizungumza na Mwananchi Kibiki amethibitisha kuondolewa katika nafasi hiyo lakini hakuwa tayari kujibu tuhuma za kuondolewa kwake.

Mkurugenzi wa mji wa Babati, Fortunatus Fwema amethibitisha kuondolewa kwa Kibiki kwenye nafasi hiyo.

 

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz