Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi za ukatili zakithiri Lindi

54916ef422934e153251fd48b046970a Kesi za ukatili zakithiri Lindi

Mon, 31 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KATI ya mashauri 652 waliyopokea wasaidizi wa kisheria mkoani Lindi, asilimia 80 ni ya ukatili, mgawanyo wa mali ya wanandoa wanapoachana na mirathi.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali Liwopac mkoani Lindi Cosma Bulu alisema hayo juzi wakati akizungumza na wadau wa sheria, wasaidizi wa kisheria na viongozi wa mashirika yasiyo ya kiserikali wa mikoa ya Lindi na Mtwara

Alisema mashauri hayo yalipokewa na wasaidizi wa kisheria, wanaosimamiwa na shirika hilo.

Alisema kwamba madai ya ardhi, mgawanyo wa mali hasa wanandoa wa napoachana, ni mashauri yanyojitokeza kila mara.

Bulu alisema kwenye vijiji vingi kuna mashauri mengi kuhusu mgawanyo wa mali ya wanandoa wanapooachana. Alisema hadi Juni mwaka huu kuna mashauri 368 yakiwemo ya ukatili dhidi ya wanawake, mgawanyo wa mali na kesi za ardhi.

Wasaidizi wa kisheria waliopo kwenye ngazi ya kata na vijiji kwa kushirikiana na shirika hilo, huwasaidia wananchi kutatua kero hizo na zinazoshindikana hupelekwa katika vyombo vya kisheria.

Mkuu wa Wilaya Lindi, Shaibu Ndemanga alisema wasaidizi wa kisheria wako chini ya Liwopac na kuna wakati muda wao utaisha.

Hivyo, alisema halmashauri za wilaya na Manispaa, ziwatambue na kuwajengea utaratibu ili watatue kero katika jamii.

Ndemanga alisema kiwango cha mashauri kimekuwa kikipungua, kwa kuwa yanatatuliwa kwa wakati, badala ya kulundika kesi mahakamani.

Alilipongeza shirika hilo kwa kufanya kazi nzuri ya kusaidia kutatua kero za jamii ngazi za vijiji na kata.

Chanzo: habarileo.co.tz