Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya anayedaiwa kumfungia mtoto kabatini, kujeruhi yapigwa kalenda

40593 KESI+PIC Kesi ya anayedaiwa kumfungia mtoto kabatini, kujeruhi yapigwa kalend

Fri, 8 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Kesi ya kushambulia mwili inayomkabili,  Anitha Kimako anayedaiwa kumfungia mtoto wa binti yake wa kazi kabatini kwa miezi mitano, imetajwa leo Alhamisi Februari 7, 2019 katika mahakama ya Wilaya ya Dodoma.

Wakili wa Serikali, Harry Mbogoro ameieleza mahakama hiyo kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Anitha ambaye alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Januari 7, 2019  anakabiliwa na shitaka la kumshambulia mwili, Neema Matimbe Desemba 27, 2018 na kumsababishia maumivu makali.

Hata hivyo,  Anitha anayetetewa na wakili,  Christopher Malinga alikana shtaka hilo mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya Wilaya ya Dodoma, Anold Kirekiano.

Kesi hiyo itatajwa tena Machi 7, 2019 baada ya upande wa mashtaka kudai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

 Soma zaidi>>Anayedaiwa kumfungia mtoto kabatini, kujeruhi afikishwa mahakamani

            >>



Chanzo: mwananchi.co.tz