Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kero ya maji Muheza kuwa historia Februari

Fe1bffb0c45d0e4f97c62f98e37ceecb Kero ya maji Muheza kuwa historia Februari

Mon, 21 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

SERIKALI imewahakikishia wakazi wa wilaya ya Muheza mkoani Tanga kuwa mpaka ifikapo Februari mwakani, watapata huduma ya uhakika ya majisafi na salama.

Hatua hiyo imekuja baada ya utekezaji wa awamu ya mwisho ya ukamilikaji wa Mradi wa Maji wa Pongwe – Muheza, unaotekelezwa na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga UWASA) kwa gharama ya Sh bilioni 6.1.

Akizungumza wakati wa akikagua miradi ya maji, Naibu Waziri wa Maji, Maryprisca Mahundi aliwataka wananchi hao kuendelea kuwa na imani na serikali yao, kwani inajitahidi kumaliza kero hiyo.

"Tunatarajia kumlipa mkandarasi malipo yake ya mwisho mapema Januari, hivyo matarajio yetu mpaka ifikapo Februari wananchi wataachana na kupata maji kwa mgao," alisema Mahundi.

Alipongeza jitihada za Tanga UWASA za kulinda na kutunza chanzo cha maji cha Bwawa la Mabayani, hali iliyosaidia kuhudumia sasa wilaya mbili za Tanga na Muheza bila ya chanzo hicho kukauka.

Aliwataka kuendelea kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira, ikiwemo uhamasishaji wa upandaji wa miti katika bwawa hilo ili liwe endelevu na wananchi waendelee kupata huduma.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga UWASA, Geofrey Hilly alisema kuwa miongoni mwa changamoto zilizokuwepo ni wananchi kufanya shughuli za kibinadamu kwenye bwawa hilo na hivyo kusababisha uchafuzi wa maji.

Meneja wa Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) mkoani Tanga, Upendo Lugongo alisema wamefanikiwa kupunguza kero ya upatikanaji wa maji kwa zaidi ya asilimia 70.

Alisema kuwa wameendelea kutekeleza kwa vitendo sera inayomtaka kila mwananchi kupata huduma hiyo kwa chini ya umbali wa mita 400.

Chanzo: habarileo.co.tz