Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaya maskini Mtwara zaomba mitaji

93ad681e704f7749ec975232f33b2862.png Kaya maskini Mtwara zaomba mitaji

Thu, 4 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

VIJANA wanaotoka kwenye kaya masikini na mazingira magumu wilayani Mtwara wameiomba serikali kuwawezesha mitaji ili waweze kuendesha shughuli zao za ujasiriamali.

Ombi hilo limetolewa jana na vijana hao wakati wa kufunga mafunzo ya mwezi mmoja kwa vijana hao wanaotoka kaya masikini na mazingira magumu kuhusu kuwaongezea ujuzi kwa kutengeneza batiki na usindikaji wa vyakula mbalimbali yaliyokuwa yanatolewa na Shirika la Viwanda vidogo(SIDO) mkoani Mtwara.

Mpango huo wa mafunzo hayo umefadhiliwa na serikali kwa kushirikiana Benki ya Dunia kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa, mradi ambao unasimamiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA).

Mafunzo hayo yameshirikisha vijana 41 kutoka kata mbalimbali wilayani humo na mchakato wa kuwapata vijana hao ulifanywa na TEA kwa kushirikiana na Mpango wa Kunusuru Kaya masikini ulio chini ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF).

Kwa upande wao vijana hao akiwemo Mwajuma Hassani kutoka Kata ya Mkunwa wilayani humo ambaye pia ni mtengenezaji wa batiki, alisema serikali ni vema ikawawezesha mitaji.

Hassan Ally kutoka Manispaa ya Mtwara Mikindani ambaye ni msindikaji wa vyakula, alisema elimu waliyoipata ni sehemu ya kuwa na ajira.

Kaimu Meneja wa SIDO mkoani hapa, Twaha Sued alisema wanufaika wa mradi huo ni kutoka mikoa 18 Tanzania Bara ikiwa Mtwara ni miongoni mwa mikoa hiyo na fedha ambazo zimetumika katika mafunzo hayo ni zaidi ya Sh milioni 36.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Danstan Kyobya, Katibu Tawala Wilaya ya Mtwara, Thomas Salala amewataka wahitimu hao wakathubu kwa vitendo kupitia ujuzi walioupata ili waweze kufikia malengo yao.

Chanzo: www.habarileo.co.tz