Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaya 92 zabomolewa Nyumba Kibaha (+Video)

Bomoa Kibaha Kaya 92 zabomolewa Nyumba Kibaha

Mon, 6 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya kaya 90 katika Kitongoji cha Matuga, Wilayani Kibaha Mkoani Pwani, zimelazimika kulala nje kwa kukosa makazi ya kuishi, kufuatia watu wasiojulikana, kuvamia na kubomoa makazi yao kwa madai ya kuwa ni agizo la Mahakama.

Wakizungumza kufuatia kadhia hiyo, wananchi hao wamesema, bomoabomoa ilianza kufanyika Jumatatu ya Januari 30 mwaka huu 2023, huku kwa mujibu wa madai yao, anayedaiwa kuwa mmiliki wa eneo hilo alikuwa na kesi dhidi ya Mwenyekiti wa Kitongoji cha Zegereni, pamoja na mtu mwingine ambaye alifahamika kwa jina la Batazali. ambao pia hawahusiki na eneo hilo lililovunjwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Nickson Simon akizungumza kwa njia ya simu kuhusu Sakata hilo, amesema wananchi ambao hawakuridhika na uamuzi huo wa mahakama wanapaswa kukata rufaa ya kupinga hukumu hiyo, huku Mbunge wa Kibaha vijijini Michael Mwakamo akieleza kigugumizi cha wananchi juu ya suala la kupinga uamuzi huo katika mazingira ambayo hawaifahamu kesi husika.

Kwa mujibu wa wananchi wa eneo hilo, Wabomoaji hao wameahidi kuendelea kubomoa kwa madai ya kutekeleza agizo, huku wakiiomba serikali kuingilia kati mgogoro huo, kutokana na wasiwasi wa kuwa, huwenda zaidi ya nyumba 100 zinaweza kuathirika na kusababisha maafa makubwa.

View this post on Instagram

A post shared by Wasafi FM (@wasafifm)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live