Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaya 77 zahama Ngorongoro

Tanzania Yalikaribisha Bunge La EU Kukagua Ngorongoro Kaya 77 zahama Ngorongoro

Tue, 19 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KAYA 77 zenye watu 463 na mifugo 1,408 waliohama kwa hiari kutoka Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Msomera wameagwa leo katika ofisi za mamlaka ya hifadhi hiyo.

Ofisa Uhifadhi Mkuu, Flora Assey ambaye ni meneja mradi wa kuhamisha wananchi wanaohama kwa hiari Ngorongoro amesema kufikia wiki hii jumla ya kaya 1,195 zenye watu 7,195 na mifugo 33,064 zimeshahama ndani ya hifadhi.

Amesema kati ya kaya 77 zilizohama ndani ya hifadhi wiki hii, kaya 75 zimeenda kijiji cha Msomera Wilaya ya Handeni na kaya mbili zimehamia kijiji cha Makao Meatu mkoani Simiyu

Naibu Kamishna wa Hifadhi Huduma za Shirika NCAA, Salum Mjema amebainisha kuwa Serikali imeendelea kuboresha zoezi la utoaji elimu, uandikishaji na uthaminishaji kwa kuongeza timu ya uandikishaji ambapo ndani ya mwezi mmoja taratibu zote ikiwepo malipo zinakuwa zimekamilika na wananchi kuhamishwa bila kusiburi mda mrefu.

Mjema ameongeza kuwa ujenzi wa nyumba za makazi 2,500 Msomera unaendelea kwa kasi ambapo nyumba 903 zimeshakamilika, nyumba 97 zipo katika hatua za umaliziaji, nyumba 1500 zipo kwenye hatua mbalimbali za ujenzi huku maandalizi ya ujenzi wa nyumba zingine 2500 yakiendelea vijiji vya Kitwai, Wilayani, Simanjiro na Saunyi Wilaya ya Kilindi. -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live