Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaya 4807 Ilemela zanufaika na TASAF

942ea8a2393b7de86424de291733fe50 Kaya 4807 Ilemela zanufaika na TASAF

Thu, 4 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

KAYA 4807 wilayani Ilemela wamenufaika na mpango wa kunusuru kaya maskini nchini(TASAF).

Hayo yalisemwa na Afisa maendeleo ya jamii manispaa ya Ilemela Frank Msafiri wakati wa kutembelea kaya mbali mbali za wanufaika. Alisema wanufaika hao idadi yao ni ndani ya kipindi cha miaka mitano(2015-2020).

‘’2015 tulianza na zoezi la uwandikishaji na lengo lilikuwa kufikia kaya 6700 lakini kaya zilizonufaika na kuandikishwa na kukidhi vigezo zilikuwa kaya 4807’’ alisema Msafiri.

Alisema lengo kubwa la TASAF,awamu ya Tatu ni kuziondoa kaya kutoka kwenye umasikini uliokithiri. Alisema katika kipindi cha 2015-2020 tumeweza kupeleka shilingi bilioni 4/- kwa wanufaika.

Msafiri alisema ruzuku wanayopokea wanufaika imegawanyika katika mafungu mawili ambayo ni ruzuku ya msingi na Ruzuku ya mashariti.

Alisema katika kila Ruzuku,wanayotoa wanahamasisha wanufaika kujiunga na uwekezaji. Alisema mwaka huu Ilemela itatoa bilioni 1/- kwa wanufaika na wanategemea kuongezeka kwa wanufaika.

Mnufaika wa TASAF kutoka kata ya Kitangiri,Pepetua Mhozya alisema kupitia ruzuku za mfuko huo ameweza kujiajiri kwa kufungua biashara ya kuuza dagaa katika soko la Kitangiri.

Alisema pia kwa fedha hizo ameweza kujenga nyumba ya vyumba vitatu na sebule.

Mnufaika mwingine, Sarah Kilinga kutoka mtaa wa medical Research alisema kupitia ruzuku za Tasaf ameweza kumsomesha mtoto wake(Yohana Mihambo) shule ya msingi na mpaka sasa ni mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Dodoma(UDOM) .

Chanzo: habarileo.co.tz