Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaulia waanzisha mfuko wa elimu

Fri, 2 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tabora. Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora imeanzisha mfuko wa elimu na kuunda bodi ya kusimamia mfuko huo unaoanza na akiba ya Sh12.5milioni.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kaliua, Dk John Pima amelieleza baraza la madiwani kuwa halmashauri hiyo imechangia Sh10 milioni huku madiwani wakichangia Sh1.4 milioni na watumishi Sh1.1 milioni.

Dk Pima amesema baraza limepitisha kuundwa kwa mfuko huo ambao mwenyekiti wa bodi atakuwa mchungaji Amos Chidemi wa Kanisa la Anglikana, katibu wake ni ofisa elimu sekondari, Daud Nkwama na wajumbe mbalimbali wakiwemo madiwani wawili.

Ameeleza malengo ya mfuko huo kuwa ni kuongeza motisha kwa walimu, uongozi wa shule na wanafunzi ambao wapo watakaolipiwa ada na matumizi mengine.

Chanzo: mwananchi.co.tz