Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kauli ya RC Makalla kwa wanaong'oa mapambo ya barabara

Makallapic Data Kauli ya RC Makalla kwa wanaong'oa mapambo ya barabara

Tue, 7 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amewaonya watu wenye tabia ya kung'oa chuma zilizowekwa barabarani kwa ajili ya kupendezesha jiji hilo.

Makalla ameyasema hayo leo Jumanne Desemba 7,2021 alipofanya ziara ya kukagua usafi wa barabara za kwenda viwanja vya ndege mkoani humo sambamba na kuwakabidhi rangi wakurugenzi wa wilaya za Dar es Salaam.

Amesema urembo huo uliwekwa kipindi cha nyuma lakini watu wenye nia ovu waliuondoa jambo ambalo kwa sasa amesema watu wa aina hiyo hawatavumiliwa.

Kuhusu ukaguzi huo amesema ni mwendelezo wa kampeni ya kuuweka mkoa huo safi baada ya kukamilisha shughuli ya kuwaondoa wamachinga kwenye maeneo yasiyo rasmi iliyopewa jina la 'Safisha pendezesha Dar'.

Katika hatua nyingine Makalla amewataka wanananchi kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho ya sikukuu ya Uhuru yatakayofanyika Desemba 9,2021 katika uwanja wa Mkapa.

"Nawaomba wananchi wa Dar mjitokeze mapema kushuhudia sherehe hizo ambapo milango itakuwa wazi kuanzia saa 12:00 asubuhi na kutakuwa na burudani mbalimbaliā€ amesema Makalla.

Advertisement

Chanzo: www.tanzaniaweb.live