Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Katibu Tawala: Mke mwenye pesa haachwi kisa mchepuko!

Happiness Seneda Katibu Tawala: Mke mwenye pesa haachwi kisa mchepuko!

Mon, 12 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Happiness Seneda amewashauri Wanawake kujiimarisha kiuchumi ili kuwa na maamuzi katika Familia huku akisema Wanawake wakiwa na fedha itakuwa ngumu kuachwa na Wanaume zao na hata kama Wanaume zao wakiwa na michepuko ila hawatowaacha wa njia kuu wenye pesa.

Amesema hayo wakati akiongea na Wanawake Wajasiriamali wa kikundi cha Tujijenge cha Wilayani Mbozi ambapo amewasisitiza kuwa wasiogope kujaribu fursa.

“Msiogope kujaribu fursa, pambaneni, umeolewa ukiwa na hela yako na kama na wewe unatoa mchango hayo mapenzi ni next level, maisha ya saa hizi usikae tu kazi yako ni kutega goli, lazima uwe na hela yako”

“Mkikaa mkianza kupanga jambo na wewe unachangia hata huyo Mwanaume atakuwa na respect anaona hili jukwaa nikiliacha litaweza kujisimamia, kwa muktadha huo hakuachi hovyo, ofcourse atakuwa na michepuko si mnajua wale Ndugu zetu (Wanaume) michepuko ndio habari yao laini ile njia kuu itabakia palepale kwa sababu unaweza kujisimamia kwahiyo tupambane kwasababu tunaweza na tuchukue fursa kipindi hiki ambacho Kiongpzi wetu mkubwa ni Mwanamke na huyu Mama (Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan) anapambana sana kutoa fursa kwa akina Mama”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live