Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Katavi yasajili wanafunzi 6,000 kuanza darasa la kwanza leo

WhatsApp Image 2022 01 16 At 3.51.56 PM (1).jpeg Katavi yasajili wanafunzi 6,000 kuanza darasa la kwanza leo

Mon, 17 Jan 2022 Chanzo: ippmedia.com

Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi imesajili wanafunzi 6000 wanaoanza darasa la kwanza sawa na asilimia 52.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tanganyika, Shabani Juma,  amesema mpaka kufikia Ijumaa Junuari 21,2022 idadi hiyo itakuwa imeongezeka kwani lengo lao ni kusajili watoto 12,000.

Shabani, amesema wako katika ukaguzi wa hatua za mwisho kukagua meza, viti, na madarasa ambapo madarasa yote 127 ya shule za msingi yamekamilika.

"Idadi ya wanafunzi wanaoingia kidato cha kwanza ni 3,053 na watoto wapo tayari kuja kesho (leo) tutafanya uhakiki, lakini baada ya wiki moja tutakua tumefikia asilimia 90 ya uandikishaji kwa shule za msingi," amesema Shabani.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Onesmo Buswelu amesema wamepita kukagua madarasa yote ya msingi na sekondari yamekamilika hivyo kila mzazi ahakikishe mtoto anafika shule.

Buswelu amesema wazazi wote wenye watoto waliofaulu kuanza kidato cha kwanza wahakikishe wanafika shule hawata mvumilia mzazi yeyote ambaye atakaa na mtoto nyumbani aliyefaulu kuanza kidato cha kwanza.

Hata hivyo Buswelu ameendelea kuwasisitiza wazazi wenye watoto wenyeumri wa kuanza darasa la kwanza na awali kuwaandikisha haraka kabla masomo hayajaanza.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Kabage, Kulwa Mahinda amesema wamekamilisha mdarasa 16 ya shule za msingi Kabage yenye thamani ya zaidi ya Sh.milioni 300.

Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi shule ya Imalaupina Mariam Awadhi amemshukuru Rais Samia Suluhu Hasan kwa kuwajali na kuhakikisha wanajenga madarasa ili watoto waweze kusoma vizuri na kufikia ndoto zao.

Chanzo: ippmedia.com