Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Katambi azindua mradi wa maji Sekondari Kolandoto

WhatsApp Image 2021 07 15 At 18.55.14.jpeg Katambi azindua mradi wa maji Sekondari Kolandoto

Fri, 16 Jul 2021 Chanzo: ippmedia.com

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, na Ajira, alisema mradi huo utasaidia wanafunzi kutunza mazingira ya shule kwa kupanda miti, pamoja na usafi.

"Mpaka sasa nimesha chimba visima viwili vya maji katika shule za Sekondari ya Mwawaza na hapa Kolandoto, ili kumaliza tatizo la wanafunzi kukosa maji shuleni, na hili nitalifanya kwenye shule zote ambazo zina changamoto ya ukosefu wa maji," alisema Katambi.

Aidha aliwataka wanafunzi kuendelea kusoma kwa bidii, ili watimize ndoto zao, huku akiahidi kuzifanyia kazi changamoto zote katika shule hiyo, ikiwamo ya upungufu wa mtundu ya choo, Walimu, Viti, Meza, na Nishati ya umeme.

Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo akiwamo  Magesa Rubinza na Salma Abdul, kwa nyakati tofauti wamesema mradi huo wa maji utakuwa mkombozi kwao, hasa katika utunzaji wa mazingira na usafi, na kuepukana na magonjwa ya mlipuko.

Alisema mradi huo wa maji umewapusha kupoteza muda wa masomo kwa kufuata maji umbari mrefu, pamoja na kubeba maji kutoka nyumbani na kufika shuleni wakiwa wameshachoka, na kutokuwa makini na masomo.



Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kolandoto, Deus Maganga, alisema mradi huo wa maji ni mkombozi katika shule hiyo, kwa utunzaji wa mazingira na usafi, na hata kuondoa adha ya wananchi ya ukosefu wa maji, ambao anaishi jirani na shule hiyo, ambapo wamekuwa wakiyatumia.

Alisema mradi huo ulianza kutekelezwa June 8 mwaka huu, na kukamilika June 12, kwa gharama ya Sh.milioni 20, kwa msaada wa Ofisi ya Mbunge Katambi, chini ya mfadhili Serving Friends International kutoka Arusha.
Chanzo: ippmedia.com