Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kanisa laiachia Serikali kifo cha Askofu Kwangu

Kifo Pic Kaburi Kanisa laiachia Serikali kifo cha Askofu Kwangu

Mon, 5 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Mahimbo Mndolwa ameiomba Serikali na vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa kifo cha Askofu Mstaafu Boniface Kwangu kilichotokea kwa njia ya kutatanisha.

Mwili wa Askofu Boniface Kwangu ulikutwa ukielea eneo linapojengwa daraja la JPM (Kigongo-Busisi) Desemba Mosi mwaka huu baada ya kupotea kusikojulikana Novemba 28, 2022.

Akizungumza leo Jumatatu Desemba 5, 2022 kwenye misa ya mazishi ya Askofu huyo mstaafu, Askofu Mahimbo amesema waniachia Serikali kushugulikia waliohusika na kifo chake

“Kama kuna aliyehusika na kifo chake tunaiachia Serikali,” amesema.

Akizungumza na Mwananchi kwa niaba ya familia nyumbani kwa marehemu eneo la Sibula Wilaya ya Ilemela Desemba 2, Mchungaji Allan Kwilasa alisema hadi sasa kifo hicho kimeacha giza nene na kitendawili ambacho kitakachoteguliwa na matokeo ya uchaguzi wa polisi.

Kwilasa alisema Askofu huyo mstaafu alikuwa ni mpole, aliyependa kuchangamana na watu na hasiye weza kuwa na adui ambaye anaweza kumdhuru kwa namna kifo chake kilivyotokea.

"Kwa maelezo ya mama Askofu (Mke wa Askofu Mary Kwangu), Baba Askofu alikuwa na safari ya kwenda Sengerema kwa shughuli zake binafsi.

“Alipanga kutumia usafiri wa gari lake kabla ya kubadilisha uamuzi kwa kumuita mmoja wa vijana wake anayeitwa Seba (Sebastian Joseph) kumfuata mjini ili arejeshe gari nyumbani," alieleza mchungaji Kwilasa namna ambavyo askofu huyo aliondoka nyumbani kwake kabla ya mauti haijamkuta.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live