Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kanisa Katoliki Geita lavamiwa na kuvunjwa

Kanisaa11 Kanisa Katoliki Geita lavamiwa na kuvunjwa

Sun, 26 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtu asiyefahamika amevamia na kuingia ndani ya Kanisa Katoliki Jimbo la Geita na kufanya uharibifu katika altare na sakrestia na kuvunja tabernakulo, kumwaga ekaristi takatifu na kuchana kitabu kitakatifu Biblia sambamba na kuharibu mfumo wa camera za ulinzi.



Taarifa iliyotolewa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita kwa njia ya simu Flavian Matindi Kasalla amesema mtu huyo alivunja kioo cha mlangoni na kuharibu madhabahu takatifu huku akiharibu sehemu mbalimbali za ibada na kuharibu vitabu vitakatifu.

“Mpaka sasa hatujajua alikotokea na wala hatujui aliingia saa ngapi japo ilikuwa ni usiku wa kuamkia siku ya Jumapili, kanisa letu linalindwa na kampuni ya ulinzi ila mpaka sasa ni kitendawili kuwa mlinzi alikuwa wapi.



Mtu aliyefanya tukio hilo amekamatwa na ameshafikishwa katika vyombo vya usalama pamoja na mlinzi aliyekuwa zamu siku hiyo” amesema Askofu Kasalla.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita ACP Berthaneema Mlayi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba watu wawili wanashikiliwa na upepelezi wa tukio hilo unaendelea.

Mpaka sasa, watu wawili wanashilikiwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi kuhusu tukio hilo.



Akithibithisha kukamatwa kwa watu hao, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita ACP Berthaneema Mlay amesema jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi zaidi ili kubaini nani kamtuma na sababu za kufanya uharibifu huo.

“Mtu huyo anaonekana alikuwa mlinzi na ni mtu ambaye amekuwa akihudumu katika kanisani haswa huko alikotoka Bukoba hivyo jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi na itakapobainika tutatoa taarifa zaidi kwani mpaka sasa kuna mambo tunayafuatilia tatutayazungumza ili kutovuruga upelelezi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live