Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni za uzoaji taka hazina uwezo - Dr. Mpango

 Dr. Philip Mpango Kj Dr. Philip Mpango

Mon, 5 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu wa Rais wa Tanzania, Dr. Philip Mpango amesema baadhi ya kampuni za uzoaji taka hazina uwezo wakufanya shughuli hiyo kwakua bado maeneo mengi ya nchi yamechafuliwa na takataka hasa za plastiki hali inayohatarisha maisha ya watu, viumbehai na kuharibu vyanzo vya maji

Dr. Mpango ameyabainisha hayo mapema leo Jijini Dodoma mara baada yakuongoza zoezi la usafi wa Mazingira eneo la Soko la Machinga katika siku ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa imefanyikia eneo hilo.

Katika hatua nyingine Dr. Mpango ameiagiza Wizara ya Nchi ,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira kwakushirikiana na wizara zingine kutafuta makampuni yanayoweza kubadilisha takataka kuwa vitu mbadala vitakavyoweza kutumika kwa matumizi mengine ili kulinda Mazingira ya watu, vyanzo vya maji na viumbe hai, huku akitaka kasi ya kuzuia mifuko ya plastiki iongezeke.

Mbali na siku ya Mazingira Duniani Makamu wa Rais Dr. Mpango aliwasikikiza wafanyabiashara wadogo wa soko hilo ambao waliomba kero zao zitatuliwe ,hali iliyomsukuma kutoa maagizo kwa Jiji la Dodoma kuweka lami mbele ya soko hilo la Machinga ,kuweka taa zinazotumia nishati mbadala ,kuweka vifaa vyakukinga jua na mvua.

Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani kwa mwaka 2023 inasema “Shinda uchafuzi wa mazingira unaotokana na taka za plastiki

Chanzo: www.tanzaniaweb.live