Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni ya bima yashitakiwa fidia ya ajali

F541ee2cb688ff992ef5dcd338b5c7ea.jpeg Kampuni ya bima yashitakiwa fidia ya ajali

Fri, 12 Nov 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ulinzi ya Geo Security ya Arusha, James Rugangira (43) ameishitaki kampuni ya bima ya Britam Tanzania Limited ya Arusha akidai fidia ya ajali.

Mfanyabiashara huyo mkazi wa Moshono jijini Arusha, anadai alipata ajali Julai Mosi, 2019 katika mzunguko wa NMC eneo la Unga Limited Arusha na alifanyiwa upasuaji wa kichwa katika hospital ya Aga Khan ya jijini Nairobi, Kenya.

Februari Pili mwaka huu Rugangira alifungua kesi ya madai namba 07/2021 katika Mahakama ya Wilaya ya Arumeru, na itaanza kusikilizwa Desemba Mosi mwaka huu mbele ya hakimu, Amalia Mushi.

Katika shauri hilo mdai anadai kuwa kutokana na ukubwa wa bima iliyokatiwa gari hilo lililopata ajali inaruhusu kulipwa

hadi Sh milioni 60, lakini kampuni hiyo ilikuwa tayari kumlipa Sh 5,000,000 hivyo alikataa fedha hizo na kufungua kesi katika mahakama hiyo.

Katika shauri hilo Rugangira anadai kuwa kampuni hiyo ilishindwa kumlipa fidia baada ya kupata ajali akiwa kwenye gari lake aina ya Toyota RAV 4 lenye namba za usajili T 828 DGN.

Alidai kuwa baada ya ajali kampuni hiyo ilipaswa kumlipa fidia ya shilingi milioni 20 kwa ajili ya matibabu aliyopata katika Hospitali ya Aga Khan nchini Kenya.

Rugangira alidai kuwa kwa sababu alikaa muda mrefu ya bila kufanya kazi alistahili kulipwa fidia ya Sh milioni 20 lakini kwa kuwa walishindwa kumlipa awali gharama zimeongezeka Sh milioni 20 nyingine. Pia alidai kuwa kampuni hiyo inapaswa kumlipa Sh milioni 100 zikiwa ni gharama za athari alizopata kwa kipindi chote.

Chanzo: www.habarileo.co.tz