Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni ya Green Miles yatia ngumu kuachia kitalu

92548 Pic+green+milles Kampuni ya Green Miles yatia ngumu kuachia kitalu

Wed, 22 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Kampuni ya Green Miles iliyotakiwa kuondoka katika i kitalu cha uwindaji cha Lake Natron (East) wilaya ya Longido mkoani Arusha kuanzia leo Jumanne Januari 21, 2020  imesema haina taarifa rasmi ya kutakiwa kuondoka.

Jumamosi iliyopita mkuu wa Wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe aliitaka kampuni hiyo kukabidhi kitalu hicho serikalini leo.

Hata hivyo, leo kaimu meneja wa kambi za kampuni hiyo,  Lazaro Lembrice amewaeleza wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Longido kuwa hawana taarifa za kufungwa kwa kambi hiyo na kwamba mmiliki wa kampuni hiyo, Awadhi Abdallah yupo nje ya Tanzania kwa muda mrefu.

“Hatuna taarifa za mkurugenzi tangu Desemba 2019, sisi tunasikia kuwa tunatakiwa kufunga kambi,” amesema.

SOMA ZAIDI: Saa za kampuni ya Green Miles zahesabika Tanzania

Katibu tawala wikala ya Longido, Toba Nguvila  aliyekuwa anaongoza ujumbe wa kamati hiyo pamoja na maafisa wa Mamlaka ya Wanyamapori (Tawa) na polisi wanaendelea na mahojiano na watendaji waliopo katika kambi za kampuni hiyo.

Pia Soma

Advertisement

Jumamosi iliyopita Mwaisumbe amesema mwaka 2019 baada ya kampuni hiyo kutakiwa kuondoka katika kitalu hicho, iliomba kuongezewa muda hadi Desemba 16, 2019 ili kukamilisha uwindaji ombi ambalo lilikubaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii.

SOMA ZAIDI: Waziri Kigwangalla afuta umiliki kitalu Green Miles Safaris, DC atoa shukrani

Amesema kampuni hiyo imeendelea kuwepo na hivi karibuni katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Profesa Adolf Mkenda alitoa taarifa nyingine akiitaka kampuni hiyo kuondoka Januari 20, 2020.

Kwa muda mrefu kampuni hiyo imekuwa na mgogoro na vijiji 23 vinavyozunguka kitalu hicho vinavyodai zaidi ya Sh350 milioni.

Pia, inadaiwa kukiuka taratibu za umiliki wa kitalu ikiwepo kushindwa kudhibiti ujangili baada ya twiga 16 kuuawa katika kitalu hicho, madai ambayo Awadh amekuwa akiyakanusha.

Chanzo: mwananchi.co.tz