Kamishina Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Geita Bw.Rugambwa Banyikila amefanya ziara ya Kushitukiza kwa Maafisa Ardhi walio katika Ofisi za Halmashauri ya Mji Geita na kukuta Lundo za Hati za wananchi zikiwa katika Meza huku akibaini uwepo wa Mchezo unaochezwa na Maafisa Ardhi hao na kutoa Maagizo hati hizo kufanyiwa kazi Mara moja na kugawiwa kwa wananchi.
Akizungumza na Millard ayo Bw. Rugambwa amesema amekuwa akiwauliza watumishi hao juu ya kuandaliwa kwa hati wamekuwa wakimjibu tayari hati zimeandaliwa jambo ambalo limekuwa halina ukweli ndani yake na Baada ya kufanya ziara amekuta lundo la hati za wananchi zikiwa katika Ofisi na bado hazijafanyiwa kazi yoyote.
“Nilishatoa Agizo mwananchi akilipia nyaraka lazima aandaliwe hati mara moja na tumetoa dedline ya wiki moja watu wote waliokwisha lipia waweze kuandaliwa hati na nimekuwa nikiwauliza hawa watumishi kwamba hati zimeandaliwa wanasema zimeandaliwa nilipofanya ziara ya kushitukiza leo hii ahsubuhi haya Majarada yote nimeyakuta katika meza zao hizi na hayajafanyiwa kazi yoyote niko hapa kuhakikisha kwamba hati za wananchi hawa zinatoka , ” Kamishina Msaidizi Banyikila.
Aidha Bw. Banyikila amesema kuna Hati ambazo zimelipiwa na zina muda Mrefu na hazijafanyiwa kazi huku akisema watumishi hao wamekuwa wakija ofisini kufanya Biashara zao na kutoa siku saba kuhakikisha nyaraka( hati) ziwegawiwa kwa wananchi.
“Tunao Mfano wa Nyaraka hizi huyu mwananchi amesaini tarehe Novemba 20, miezi mitano iliyopita bado Jarada liko hapa tukiuliza nini sababu hatuna sababu tumepewa hizi dhamana tuwasaidie wananchi wetu ko ni vizuri kuhakikisha kwamba na hapa hakuna shida kuna wateule wawili nilijaribu kuongeza mteule ili kuhakikisha kazi zote zinatoka kwa wakati, ” Kamishina Msaidizi Mkoa wa Geita, Banyikila.
Bw.Banyikila amesema ataendelea kufanya Ziara ya Kushitukiza katika Halmashauri zote zilizopo ndani ya Mkoa wa Geita na endapo atabaini uwepo wa lundo za hati za wananchi Ofisini atawachukulia hatua kali za kisheria huku akizitaka Halmashauri zingine kuiga Mfano wa watumishi kutoka Halamshauri ya wilaya ya Mbogwe.