Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamati ya RC Mghwira yaondoka na DC Mwanga

38763 DC+PIC Kamati ya RC Mghwira yaondoka na DC Mwanga

Tue, 29 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Unaweza kusema kamati ya uchunguzi iliyoundwa na mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira kuchunguza mgogoro wa uongozi wilayani Mwanga umeondoka na Aaron Mbogho.

Mbogo alikuwa mkuu wa Wilaya hiyo lakini jana Jumapili Januari 27, 2019 Rais John Magufuli alitengua uteuzi wa Mgogho na nafasi yake kuchukuliwa na Thomas Apson.

Kamati hiyo iliyoundwa na Mghwira ilipendekeza, kati ya  Mbogho na mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya hiyo, Zefrin Lubuva waondoke wote wawili au mmoja kwa maelezo kuwa wasipokuwa pamoja kazi itafanyika vyema.

Juzi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika kikao cha wakuu wa Mikoa jijini Dodoma, alionyesha kushangazwa na kitendo cha baadhi ya viongozi wa serikali kushindwa kuelewana na kufikia hatua ya kupigana ofisini, kubainisha kuwa jambo hilo ni aibu wa Taifa.

 

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi



Chanzo: mwananchi.co.tz