Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamati kuundwa kuchunguza moto ulioteketeza soko Karume

Moto Kamatiii Kamati kuundwa kuchunguza moto ulioteketeza soko Karume

Sun, 16 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC), Amos Makalla amewataka wafanyabiasha wa soko la Karume lililoungua kuwa watulivu huku akiahidi kuundwa kamati itakayochunguza kujua chanzo cha moto huo.

Makalla amesema hayo leo Jumapili Januari 16, 2022 alipotembelea eneo hilo na kukagua athari za moto huo.

Soko la Karume (soko la mchikichini) liliteketea moto usiku wa kuamkia leo huku chanzo cha moto huo kikiwa hakijulikani.

Imeelezwa kuwa moto huo ulioteketeza sehemu kubwa ya soko hilo lenye wafanyabiashara zaidi ya 3,500 ulianza usiku wa kuamkia leo huku Jeshi la Zimamoto na Uokoaji likijitahidi kuuzima lakini uliteketeza soko hilo sehemu kubwa.

Akiwa akiwa kwenye eneo hilo Makalla amesema "Nawapa pole wafanyabishara wote kwa ajali hii ya moto hatujajua chanzo kwa kuwa yanaelezwa mengi, wengine wanasema umesababishwa na watu wanaopika maharage usiku ili wakifika asubuhi yameiva. Nawaomba kuweni watulivu katika kipindi hiki ambacho tunaunda kamati itakayochunguza kujua chanzo," amesema

“Tutaaunda kamati itakayoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala kuchunguza kwa siku 14 kisha tutapokea majibu na kujua cha kufanya na wakati wote wa uchunguzi hakuna mfanyabiashara atakayeruhusiwa kuendelea na biashara katika eneo hili tutaangalia utaratibu mwingine,"amesema

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Wilaya ya Ilala, Elisa Mugisha amesema taarifa za moto huo walizipata baada ya kupigiwa simu na mtu mmoja.

"Na kwa bahati nzuri wakati huo tulikuwa tunatoka Mabibo ambako nako kuna nyumba ilikuwa inaungua moto na tulifika hapa ndani ya muda mfupi tulifika eneo la tukio lakini moto ulikuwa mkali kutokana na asili ya bidhaa wanazouza hapa mbao, maturubahi na nguo na vinasambaza moto kwa haraka tulijitahidi kuzunguka soko na kuanza kuzima,"amesema

Amesema vibanda vimeungua kwa asilimia 98 na mali zilizokuwemo na niwachache waliofanikiwa kuokoa bidhaa zao hasa walioko pembezoni mwa soko.

"Tunachoshukuru Mungu hakuna madhara kwa binadamu na wala moto haukuvuka kwenda kwenye nyumba za wananchi kwa sababu tulikuwa na gari nne moja kutoka Kinondoni,Ilala, Bandari na Airport," amesema

Chanzo: www.tanzaniaweb.live