Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamanda wa Polisi apiga marufuku kuwafukuza wahalifu

Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Geita, Safia Jongo.jpeg Kamanda Jongo.

Fri, 17 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Safia Jongo amepiga marufuku serikali za vijiji pamoja na polisi jamii kupitisha azimio la kuwafukuza watuhumiwa wa uhalifu kwenye maeneo yao badala yake wafuate sheria.

Kamanda Jongo amesema hayo kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Ihushi kata ya Shabaka wilayani Nyang’hwale ambapo alieleza maazimio ya aina hiyo yanaminya haki ya mtanzania kuishi nchini kwake.

“Kama mtu amekosea taratibu za kisheria zifuatwe lakini siyo kumuwekea azimio, kama ni kosa la jinai amefanya mpelekeni polisi kutengwa kwake ni kufungwa lakini siyo kumuwekea azimio la kumuhamisha.

“Hii nchi ya Tanzania kila mtu ana uhuru wa kuishi, sasa mnampigia kura mwizi na hamna ushahidi wowote juu ya tuhuma hizo, lakini mnamuazimia ahame kwenye kijiji hiyo siyo sahihi.”

Amesema polisi jamii maarufu kama sungusungu hawana madaraka ya kuazimia hukumu yeyote juu ya mtuhumiwa badala yake wasaidie jeshi la polisi kukamilisha ukamataji na uchunguzi wa watuhumiwa wa uhalifu.

“Askari kata wapeni elimu sungusungu kwamba wasijichukulie sheria mkononi kupitiliza, sugungusungu akishamshika mtuhumiwa ni zaidi ya mwanajeshi.

“Hivi vitu tunavikataa, mshike mtuhumiwa mpeleke kwenye vyombo vya sheria, kama mnasheria ndogondogo za kata basi zisiwe zinakinzana na zile sheria mama.” Amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live