Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamanda Mpinga ametaja Waliokamatwa na Meno ya Tembo yenye Thamani ya Milioni 33

3268 Mpinga 660x400

Thu, 15 Feb 2018 Chanzo: millardayo.com

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya Mohammed Mpinga amezungumza na waandishi wa habari leo February 14, 2018 kuhusu Polisi kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu wakiwa na nyara za Serikali ambazo ni vipande vinne vya meno ya Tembo.

Mpinga amewataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni Kenedy Lupembe Simsokwe ambaye Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha SAUT – Tawi la Mbeya, Mathew Elikana Mwanjala ambaye ni Mpiga picha na Shaban Mkwiche.

“Nimefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu wakiwa na Nyara za Serikali, ambapo ni vipande vinne vya Meno ya Tembo, taratibu za kisheria zinafanyika ili Watuhumiwa wafikishwe Mahakamani” -Mpinga

MAAGIZO ALIYOYATOA DC ARUSHA YA BILIONI 3 KWA HALMASHAURI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

Chanzo: millardayo.com